Ijumaa 29 Mei 2026 - 15:00
Rais wa Jumuiya ya Kisheria ya Mashia wa Jammu na Kashmir: Taifa la Iran ni Taa ya Njia kwa Umma wa Kiislamu katika Njia ya Kusimama Imara na Utukufu

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Hassan Mousavi amesema kuwa taifa kubwa la Iran chini ya vikwazo vikali zaidi, mashinikizo na njama za maadui wa Uislamu, halikurudi nyuma hata kidogo, bali kwa kuitegemea imani na utambulisho wake wa kidini limeendelea kulinda malengo halisi ya Kiislamu na mhimili wa muqawama.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Hassan Mousavi, rais wa Jumuiya ya Kisheria ya Mashia wa Jammu na Kashmir, katika hotuba yake ndani ya Husseiniyya ya “Budgam”, alisema kuwa; taifa kubwa la Iran chini ya vikwazo vikali zaidi, mashinikizo na njama za maadui wa Uislamu, halikurudi nyuma hata kidogo, bali kwa kuitegemea imani na utambulisho wake wa kidini limeendelea kulinda malengo halisi ya Kiislamu na mhimili wa muqawama.

Aliendelea kwa kutoa heshima kwa nafasi ya juu ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah al-Udhma Khamenei (qs), pamoja na kuhuisha kumbukumbu za mashahidi watukufu wa Mapinduzi ya Kiislamu, na akasisitiza kwamba; mwenendo wa mapambano na ustahimilivu wa taifa la Iran mbele ya kambi ya ubeberu ni mwongozo ulio wazi kwa mataifa yote ya Kiislamu.

Iran; Mshindi katika Medani ya Kukabiliana na Njama

Mwanazuoni huyu mashuhuri wa Kashmir huku akirejelea mashinikizo ya kila upande ya maadui dhidi ya mfumo wa Kiislamu alisema: Taifa kubwa la Iran chini ya vikwazo vikali zaidi, mashinikizo na njama za maadui wa Uislamu, halikurudi nyuma hata kidogo, bali kwa kutegemea imani na utambulisho wake wa kidini limeendelea kulinda malengo halisi ya Kiislamu na mhimili wa muqawama.

Aliongeza kuwa: Idi ya kweli ni ya taifa la Iran; kwa sababu kusimama kwao imara katika kulinda maadili ya Kiungu ni ushindi mkubwa zaidi, kujitolea kwa mashahidi wa Uislamu, hususan mashahidi wa Iran, ni hazina kubwa na jambo la fahari kwa Umma mzima wa Kiislamu.

Kilio cha Kutetea Wanaodhulumiwa Ghaza na Ulazima wa Umoja wa Kiislamu

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Hassan Mousavi, katika sehemu nyingine ya hotuba yake alizungumzia mgogoro wa kibinadamu huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na huku akionesha huzuni kubwa juu ya maafa yanayoendelea katika Ukanda wa Ghaza, aliutaka ulimwengu kuchukua hatua za haraka na madhubuti za kusitisha jinai za utawala wa Kizayuni.

Alisisitiza: Leo ni wajibu kwa Waislamu wote kusimama kwa mshikamano mmoja katika kutetea haki ya kujitawala na uhuru wa wananchi madhlumu wa Palestina. Ushindi wa Gaza unategemea umoja na mshikamano wa kivitendo wa ulimwengu wa Kiislamu.

Mwisho wa hotuba yake, rais wa Jumuiya ya Kisheria ya Mashia wa Jammu na Kashmir aliomba dua kwa unyenyekevu kwa ajili ya ushindi wa mataifa madhlumu, nguvu ya ulimwengu wa Kiislamu na kupatikana kwa amani ya kudumu duniani, pia akisisitiza umuhimu wa umoja miongoni mwa Waislamu, alimwomba Mwenyezi Mungu kudumisha hali ya undugu, udugu wa Kiislamu na usalama katika eneo la Jammu na Kashmir.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha